Mito ni pambo muhimu sebuleni inaweza kuchangamsha rangi kwa sofa zenye rangi za kupooza. Pia inaongeza faraja katika nyumba yako uwangaliapo, sofa nyingi zinakuja na mto mmoja au miwili lakini unaweza kuongezea ikawa mingi kwa kadri unavyotaka kutokana na sebuleni yako. Mito inapendezesha na unaweza kubadili ya rangi tofauti tofauti kuleta muonekano wa sebule.ila inachangamoto moja ambayo Kama utaweka mito mingi inatakiwa unaponyanyuka kwenye sofa kurudishia vizuri.
Pamoja Kuwa ni mito ni mapambo pia hutumika kwa ajili ya usingizi wa mchana wakati ambapo unahitaji mmoja kulala chini kwa dakika chache. Weka mto mgongoni uegeme kama hupendi nafasi ya kiti ulichokalia. Mtoto mdogo anaweza kukalia mto wa sofa kumsaidia akae mezani.
Mito ya kwenye sofa inaweza kuwa laini au migumu ila ni vizuri kutumia mito laini ya pamba sababu ni soft, Pia unaweza kuifua kirahisi pindi inapochafuka.
NB:
Kama budget yako inabana sana ni kiasi cha kununua mito plain bila folonya kisha nenda kariakoo katakitamba kizuri ambacho kitaendana na sofa zako na pazia kisha mpe fundi akushone hapo utakuwa umesave kiasi cha pesa.
kwa mawasiliano email.hmdecoration2010.blogspot.com













