Rangi ya kuchagua kwa ajili ya sofa za sebuleni yako.

Sio wote tunauwezo wa kwenda dukani kununua sofa mpya, kwa wale ambao kipato chetu cha kawaida ila tuna wish kupata sofa km hizo hapo chini kwenye picha  na rangi zake ni vizuri.unachoweza kufanya  kwenda dukani kununua kitamba  unachokipenda na kumpelekea fundi na sample ya sofa unalolipenda.Pili kilakitu kinapatika madukani  km utapenda style hapo chini ni vizuri utakapo kwenda kwa fundi msisitize akutole kile kitu roho inapenda vizuri pillows  za  kuegemea ukaweka pamba au sufi na zinapatika kariakoo kwa wingi tu.





Maybe red is the right color !!Rangi nyekundu ni rangi yenye ishala ya upendo,pili ni rangi ambayo itakufanya kurelax baada ya kuchoka na kazi za siku nzima ofisini.hii rangi inapendeza kwa wale wenye vyumba vidogo na vikubwa  hii ni rangi  nzuri zaidi.ukijuwa kucheza nayo. Good luck !!!


Wengi wetu tunaona ugumu kuweka sofa ya rangi ya machungwa,Kiu kweli rangi yake inapendeza sana kuweka katika room yako hakuna haja ya kuofia rangi. Rangi hii ni nzuri na inapendeza katika room yako.Hivyo mawazo yako yatakuwa makini tu kwenye sofa ya rangi ya machungwa,Tupia vimito vidogo vya machungwa kufanya sofa yako kuwa nzuri tu ni rangi zuri katika nyumba yako.




Kwa wale wanaopenda sofa za L shape ningependa kuwambia kwamba ili sofa linapendeza  kutokana na mkato wa chumba, Before ya kwenda kununua sofa la L shape angalia kwanza chumba chako kinamkato gani kisha ndio toa maamuzi.Pili ni sofa ambalo ninapendeza sana  ata kwa wale wenye vyumba vidogo sababu alichukui nafasi kubwa sana. 



Kwa ushauri na maoni email me:hmdecoration2010.blogspot.com